Sitowachekea wachafuzi wa Mazingira - Mh.Mahenge
Na Rashda Swedi- VPO
Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina
budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratibu na sheria za utunzaji wa
Mazingira.
Hayo yamesemwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais - Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge
alipofanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta (Murza
Oil Mills Limited) kilichopo Vingunguti.
hata hivyo Mheshimiwa Mahenge alisema hayo baada ya kutoridhishwa na
mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo
wa maji taka kwa lengo la kulinda mazingira kwa sababu wasipofanya
hivyo Serikali itachukua hatua ya kukifunga kiwanda hicho