Benki
kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari
inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi
mia tano haitatumika tena kuanzia Desemba 31, 92016; sio taarifa ya
kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Ukweli
ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko
sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka
mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.
Marcian Kobello.
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .
No comments:
Post a Comment