Monday, April 14, 2014

MWANA MUZIKI MKONGWE TZ AFARIKI DUNIA

R.I.P MUHIDIN GURUMO
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi nchini Tanzania ambaye alitangaza kustaafu mwaka uliopita Muhidin Maalim Gurumo amefariki dunia leo April 13, 2014 saa 9 Alasiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa kutoka kwa meneja wake zinasema kuwa Marehemu mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na taizo la mapafu kujaa maji.

JE WEWE UNA WIVU KATIKA MAPENZI, SOMA HAPA UJUE ZAIDI


Wiki hii nimeona ni vyema tukabadilishana uzoefu juu ya suala zima la wivu katika mapenzi. Mtakubaliana nami kuwa suala la kuwa na wivu kwa mpenzi wako ni jambo lisilokwepeka hasa kwa sababu kubwa ya kuaminika kwake kwamba kuwa na wivu ni moja ya kigezo cha kuonesha ni jinsi gani unampenda mpenzio na kwamba hauko tayari kwa namna yoyote ile kushea na mwingine ndio maana wanawake wengi hawataki kusikia suala la ukewenza kabisaa! Hata kama jambo hilo limepewa baraka zote na dini au tamaduni zao.
Lakini kubwa katika wivu ni ile kutokuwa tayari kuona tunasalitiwa na wapenzi/wanandoa na hasa kwa wale tunaowapenda ukweli toka moyoni mwetu na zaidi ukute ndo tumeshawagharamikia kiasi cha kutosha na kujitoa kwao kwa kila kitu!
Umeshawahi kusikia kauli kama “Jamani mke (au mume) anauma! Au kauli kama mke wa mtu sumu” na hugeuka sumu kweli hasa pale “unapobambwa” na mali za wenyewe, kufanyiwa “kitu mbaya” inakuwa sio jambo la ajabu sana.
Niwaambie kitu wapenzi wasomaji! Mapenzi bwana ni “full uchoyo, ni full kujipendelea! Mpenzi wanaume kwa mfano, anaweza kufikiria kwamba ni yeye tu ndiye anayestahili na anayeweza kumfanya mpenzi wake acheke na kufurahi.
Na kwamba akitokea mwanaume mwingine akapata nafasi ya kumfurahisha mpenzi huyo hata katika stori za kawaida tu, unaweza ukasikia akisema, “Hivi wewe mna nini na huyo jamaa, mbona unamchekea chekea hivyo, au…!” Hiyo ndiyo choyo ya penzi, na kikubwa kinachofanyika hapo ni ile tu kujaribu kulinda maslahi binafsi.


Pamoja na ukweli kwamba tabia ya wivu inapozidi hugeuka kuwa kero, lakini kabla hatujafika huko hebu tuangalie nafasi ya wivu katika mapenzi yetu. Yaani swali ni kwamba, je! Wivu katika mapenzi unaleta maana?
Nionavyo mimi wivu ukitumika vizuri unaleta maana na una nafasi muhimu sana katika mapenzi kwa sababu zifuatazo:

RAISI JAKAYA KIKWETE AONGAZO KUMBUKUMBU YA MAREHEMU SOKOINE

Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi na wajane wa hayati Edward Moringe Sokoine pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa katika misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.