Kuna nyuki wa kwenye mashine za kusaga na kukoboa. Ukiwaona ni nyuki lakini si kama wale uliowazoea. Nyuki wa mashineni hana madhara, unaweza kumkamata kwa mikono. Na wala, haenezi homa ya dengue ukashindwa kutembea kwa kudengua.
Lakini, nyuki wa mashineni anabaki kuwa nyuki. Mwanadamu utakuwa mjinga ukidhani kuwa ni sawa na nzi. Hata nyuki wa mashineni hakumbatiwi. Maana, nyuki anabaki kuwa ni nyuki tu. Busara ni kuwa na tahadhari nae.
Mtafakari nyuki wa mashineni...
Ni Neno Fupi La Leo.
Maggid,
Iringa.(P.T)
No comments:
Post a Comment