Sunday, June 1, 2014

SHEKH SHARIF, AKIFANYA MAMBO.

DSC 1650 693cb

 Akionyesha ishara ya kuombea wenye maradhi ya saikolojia.

AMFUNGA MAMA YAKE MZAZI MIAKA 2

“Siwezi kukupa comment (maoni) kwa sababu lipo kwenye uchunguzi maana suala hili nimewapatia polisi walifanyie uchunguzi, kwa hiyo wakishamaliza utaratibu wa kuchunguza wakapata ukweli wa hili jambo watanipa taarifa hivyo nitakuwa kwenye position (nafasi) ya kusema kwa hiyo nategemea kuletewa taarifa kamili kwa maandishi,” anasema Kilasi.
Hata hivyo Evaristo Ng’ande, kijana anayedaiwa kumfungia ndani mama yake huyo wa kambo alipotafutwa kutolea ufafanuzi suala hilo alisema hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa ameshatoa maelezo polisi hivyo anasubiri polisi wakamilishe uchunguzi wao wampeleke mahakamani.
“Yaani habari za mgonjwa huyo mimi siwezi kusema chochote maana maelezo yangu nimeshatoa polisi na kesi yangu iko polisi, kwa hiyo nasubiri wakamilishe uchunguzi wao nipelekwe mahakamani,” alisema Ng’ande kwa kifupi.

Ban Ki Moon ampongeza JK katika kupugania Afya ya Mama – Mtoto


Secretary-General Ban Ki-moon meets with H.E. Mr. Jakaya Mrisho Kikwete (President, TANZANIA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.(Picha na Maktaba).
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesifu jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  mchango wake mkubwa katika kupigania Afya ya Mama na Mtoto.
Bw. Ban Ki Moon ametoa pongezi hizo tarehe 30 Mei,2014 wakati alipokuwa akizungumzia  juhudi za kumuokoa Mama na Mtoto baada ya Mwaka 2015, mwishoni mwa mkutano wa siku 3 kuhusu Afya ya Mama na Mtoto kama ilivoainishwa katika Malengo ya Milenia .

VIJANA WAASWA KUACHA KUJIINGIZA KATIKA MAPENZI KATIKA UMRI MDOGO.

PIX 3 (2)
Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni “Athari za ndoa za utotoni” wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo hicho.

WAISILAMU ZAIDI YA 300, WACHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA.

1_22af5.jpg 
Naibu amir ibrahim, akiongoza kwa kutoa damu katika hospitali ya mkoa wa lind

PETER MUTHALIKA, AAPISHWA KUWA RAIS MPYA WA MALAWI.


Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7

ZAIDI YA ASILIMIA 20 YA WALIMU, WANAWANYWESHA MATONGO POLI WANAFUNZI,

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiahidi kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha, imebainika kuwa asilimia 25 ya walimu huwafundisha wanafunzi mambo yasiyo ya msingi.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), iliyozinduliwa Dar es Salaam hivi karibuni, imebainisha kuwa wakati wananchi wakilalamika kuwa elimu inayotolewa haimsaidii mwanafunzi kupata ajira nzuri, wanafunzi hawajifunzi mambo ya msingi yatakayowasaidia kupambana na changamoto za maisha.(FS)