Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.(Picha na Maktaba).
Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa amesifu jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
mchango wake mkubwa katika kupigania Afya ya Mama na Mtoto.
Bw. Ban Ki
Moon ametoa pongezi hizo tarehe 30 Mei,2014 wakati alipokuwa
akizungumzia juhudi za kumuokoa Mama na Mtoto baada ya Mwaka 2015,
mwishoni mwa mkutano wa siku 3 kuhusu Afya ya Mama na Mtoto kama
ilivoainishwa katika Malengo ya Milenia .
Rais
Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada Bw. Stephen Harper, kwa miaka minne
wamekuwa Wenyeviti Wenza wa Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji katika
masuala ya Afya ya Mama na Mtoto , ambayo imekuwa mstari wa mbele
kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga na Mama wajawazito vinapunguzwa
kwa nusu ifikapo Mwaka 2015.
“Napenda
kumpongeza Rais Kikwete kwa mchango wake mkubwa katika jitihada hizi za
kupunguza vifo vya Watoto na akina Mama. Rais Kikwete na Waziri Harper
wamedhihirisha uongozi katika kukuza Afya ya Mama na Mtoto, nawapongeza
sana “ Bw. Ban Ki Moon amesisitiza na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano wa Canada wa kuchangia zaidi katika jitihada hizi.
Pamoja na
mafanikio hayo, Rais Kikwete amesema bado jitihada zinahitajika katika
kuhakikisha mafanikio haya yanaimarishwa zaidi na kwamba hayapotei .
“Bado tunahitaji wataalamu wa Afya wenye ujuzi , vifaa na teknolojia ya kisasa” Amesema na kuongeza kuwa bado zinahitajika juhudi za pamoja katika kusimamia mafanikio yaliyokwisha kupatikana.
Bw.Ban Ki
Moon pia amesema Afya ya Mama na Mtoto ni ajenda muhimu kupigania hata
baada ya Mwaka 2015 kwani ni muhimu kwa maendeleo.
Rais
Kikwete pia amehudhuria chakuala cha jioni kilichoandaliwa na wafanya
biashara wa Canada na Tanzania ambapo ameelezea umuhimu wa biashara na
uwekezaji nchini kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa Tanzania.
Rais
amesema Tanzania inahitaji vitega uchumi zaidi kutoka Canada na hivyo
kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Canada kuja kuwekeza
Tanzania.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka Toronto leo tarehe 31 Mei, kurejea Dar es Salaam, kupitia Marekani.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Toronto – Canada.
31 Mei, 2014
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Toronto – Canada.
31 Mei, 2014
No comments:
Post a Comment