“Siwezi
kukupa comment (maoni) kwa sababu lipo kwenye uchunguzi maana suala
hili nimewapatia polisi walifanyie uchunguzi, kwa hiyo wakishamaliza
utaratibu wa kuchunguza wakapata ukweli wa hili jambo watanipa taarifa
hivyo nitakuwa kwenye position (nafasi) ya kusema kwa hiyo nategemea
kuletewa taarifa kamili kwa maandishi,” anasema Kilasi.
Hata
hivyo Evaristo Ng’ande, kijana anayedaiwa kumfungia ndani mama yake
huyo wa kambo alipotafutwa kutolea ufafanuzi suala hilo alisema hawezi
kuzungumza chochote kwa kuwa ameshatoa maelezo polisi hivyo anasubiri
polisi wakamilishe uchunguzi wao wampeleke mahakamani.
“Yaani
habari za mgonjwa huyo mimi siwezi kusema chochote maana maelezo yangu
nimeshatoa polisi na kesi yangu iko polisi, kwa hiyo nasubiri
wakamilishe uchunguzi wao nipelekwe mahakamani,” alisema Ng’ande kwa
kifupi.
Hata
hivyo baada ya maelezo hayo baadaye kijana huyu alipiga simu kwa mmoja
wa waandishi wa gazeti hili, na kumweleza kuwa hajamtelekeza mama huyo
bali kinachofanyika ni majungu kutoka kwa baadhi ya majirani zake
wasiopenda maendeleo.
“Unajua
kaka hapa Igwachanya pana majungu sana ila mama mdogo sijamterekeza na
hana mtoto mwingine wa kumtegemea zaidi yangu mimi, ni kweli hili duka
ni lake na nyumba yake ila kulingana na mazingira uliyomkuta nayo hawezi
kukaa kwa sasa dukani, hata hivyo mimi nimeweka hela zangu nyingi tu
maana lilikuwa na mtaji usiozidi milioni mbili na nusu na huwa nampa
taarifa za mauzo,” anasema.
No comments:
Post a Comment