Monday, December 26, 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA SAKATA LA MWANDISHI WA HABARI.

Sakata la mwandishi wa habari wa ITV Halfan Lihundi kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 24 kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Arumeru baada ya kuandika habari ambayo haikumfurahisha mkuu huyo, limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuingilia kati na kusema waandishi wa habari wanao uhuru wa kuandika habari mahali popote katika mkoa huo ili mradi wazingatie weledi katika taaluma.

Gambo ambaye wakati sakata hilo linatokea alikuwa safarini analazimika kukutana na wanahabari wote wa jiji la Arusha baada ya tukio hilo lililogoga vichwa vya waandishi mkoa wa huo na kusababisha kusimamisha shughuli zao ikiwemo kuweka kalamu chini kumnusuru mwenzao lakini pia wadau mbalimbali tasnia ya habari kukerwa na kitendo hicho.

Gambo amesema anatambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari na kuongeza kuwa kabla ya kiongozi huyo hajafanya maamuzi hayo pamoja na mamlaka aliyonayo busara ilitakiwa itumike.

No comments:

Post a Comment