Friday, April 11, 2014
HABARI MOTOMOTO: RONALDO KUKOSA FINALI YA COPA DEL FEY
HABARI MOTOMOTO: RONALDO KUKOSA FINALI YA COPA DEL FEY: Stori ambayo imethibitishwa na club ya Real Madrid ni kwamba staa wao Cristiano Ronaldo hatocheza kwenye mechi ya fainali ya Copa del R...
HII KALI YA MWAKA
Hii video hapa chini ni ya mama aliekua akihojiwa kwenye TV lakini ghafla akatokea mwizi na kutaka kupita na mkufu wake wa gold, mkufu huo haukua rahisi kunyofoka hivyo mwizi akakimbia na mikono yake mitupu.
Yani wezi kuibia watu ovyoovyo tu town imekua ni kitu cha kawaida kabisa kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini.
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA MICHEZO,
SIASA,
SIASA. ULIMWENGU. KITAIFA
Walichosema Mbeya City dhidi ya tuhuma ya kuhongwa na Azam FC
Taarifa waliyoitoa inaanza kwa kusema >>
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo
wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa
kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea
ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki
katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu
yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya
kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo
dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom
kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa
mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za
kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu
nchini tumezishuhudiaChangamoto hizo ikiwemo upangaji wa ratiba usiokuwa
na uwiano mzuri.
Baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo, wizi wa
mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,
uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira
katika ngazi zote n,k.
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA MICHEZO,
SIASA. ULIMWENGU. KITAIFA
RONALDO KUKOSA FINALI YA COPA DEL FEY
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA MICHEZO,
MICHZO
Sentensi 12 za alichosema Juma Duni Haji kwenye bunge la katiba leo.
Kuna wajumbe wanasema kuirudisha serikali ya Tanganyika ni kufufua makaburi, kwani imezikwa? ninachofahamu mimi Tanganyika imekufa kwa kubadilisha jina tu.
Wengine eti serikali3 zitarudisha usultani Zanzibar, Loooooh! Mashaaalah, baada ya miaka 50 tunayazungumza haya? katiba ya sasa kifungu 98b kimetoa ruhusa Watanganyika na Wazanzibar wakikubaliana muungano utavunjika sio lazima serikali 3.
Mabunge ya sasa yana wajumbe wasiopungua 438 ya serikali 3 yatakua na 314 sasa mtu anaibuka tu na kusema serikali 3 gharama.
Ikaelezwa Zanzibar kuruhusiwa kutafuta misaada nje kwa nini mliizuia sasa baada ya serikali 3 mmerejesha? ikaelezwa pia mafuta kuondolewa ktk orodha ya mambo ya muungano, ni miaka7 hii lilipitishwa, kisa serikali 3 ndio mnaliondoa?
Katika dharau tunayofanyiwa kwa udogo wetu Znz tunaambiwa hatuna uwezo kuchangia muungano, pato la Mznz na Mtanganyika halina tofauti, Tanganyika ni kubwa lakini kwa mmojammoja umasikini wetu ni sawasawa
Makusanyo ya muungano yanayotumika kwa muungano hayajazidi 35% ambapo si chini ya 60% yaliyobaki yanatumika Tanganyika, hizi tume ambazo haziundwi na account kutofunguliwa ni kwa sababu mapato haya Znz haitakiwi kupata.
Sifa ya Zanzibar kwa miaka 50 kama serikali hizi mbili kweli zilikua na nia njema, Zanzibar ingekua sasa Hongkong ya Afrika.
Znz haina benki kuu wala sarafu yake na sera zote za uchumi ziko chini ya Muungano, Zanzibar mmeifunga miguu na mikono, leo kutatua matatizo ya Muungano kwa mfumo wa serikali 3 linatangulizwa swala la gharama, kwani lini zilikua ndogo?
Nilisoma kwenye magazeti miaka 50 uhuru wa Tanganyika si chini ya Bilioni 70 zimetumika katika sherehe, sherehe zenyewe za uwanja wa taifa kutazama gwaride watu wanavyorusha viatu, hayo hayo miaka yote.
Mikoa ya Tanganyika wakati wa 64 ilikua 17 tu ila sasa haipungui 26, Wilaya zilikua 60 mpaka 70 lakini sasa hazipungui 150, kila ukipanua madudu haya unaongeza gharama za utawala, yanatuhusu nini sisi Wazanzibari magharama haya?
Alichofanya Warioba ni kujaribu kusahihisha haya ya miaka 50, baada ya kutusaidia wengi mnataka hali hii iendelee?
Hayo ndio yaliyowasilishwa na Juma Duni Haji, ya Ummy Mwalimu yanafata muda sio mrefu… ila unaweza kuacha maoni yako hapa chini kuhusu haya ya Juma Haji.
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA MICHEZO,
KITAIFA,
SIASA,
SIASA. ULIMWENGU. KITAIFA
Thursday, April 10, 2014
PATA HABARI KUHUSU MTOTO ALIYE NASWA NA RISASI KICHWANI KATIKA SHAMBULIO NAIROBI KENYA.
Inasemekana mama huyu aliuwawa kwa risasi akiwa kamkinga mwanae asipatwe na risasi lakini hata hivyo risasi hiyo ilimuua mama na kwenda kutua na kubaki kwenye kichwa cha mtoto Satrin ambae alikimbizwa hospitali na siku kadhaa baadae risasi ikatolewa
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA,
KIMATAIFA MICHEZO
KATUNI ZA KIPANYA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA.
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA,
MICHZO,
SIASA. ULIMWENGU. KITAIFA
Location:
Tanzania
Wednesday, April 9, 2014
MATOKEO YA MWANZO YA JIMBO LA CHALINZE
Tuesday, April 8, 2014
DK. SLAA: UPINZANI WETU HAUNA NIA YA KUVUNJA MUUNGANO
Na Hudugu Ng'amilo
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amewataka
Watanzania kutambua kuwa hakuna chama cha upinzani ambacho kina lengo la
kuvunja Muungano bali yanayoelezwa ni njama ya kudhoofisha msimamo wa
kuwapo kwa serikali tatu.
Alitoa
kauli hiyo jana katika viwanja vya Tangamano, alipokuwa akiwahutubia
wakazi wa jiji la Tanga, baada ya kuongoza timu ya viongozi wa juu wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) mjini hapa na kuwataka wakazi wa
jiji hilo kukataa hadaa zinazofanywa kwa lengo la kukanyaga rasimu ya
katiba, ambayo waliitolea maoni yao.
Alisema
kilichofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wakati akilihutubia Bunge Maalumu
la Katiba kuiponda rasimu ya katiba ni kumdhalilisha aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambaye
ni kiongozi mwenye heshima Tanzania na nje ya nchi na kwamba, Ukawa
itazunguka nchini kote kumtetea.
Dk. Slaa
ambaye ni Mwenyekiti wa Ukawa nje ya Bunge hilo, alisema Rais Kikwete
anawahadaa wananchi anaposema wanaotaka serikali tatu wana lengo la
kuvunja Muungano na kusisitiza kuwa hakuna chama chochote cha upinzania,
ambacho kinataka Muungano uvunjike.
"Chadema,
CUF, NCCR Mageuzi na wananchi wote wa Tanzania Bara na hata visiwani,
hakuna anayetaka Muungano uvunjike, bali kinachofanywa na CCM ni
kuwachonganisha kwa wananchi ili waonekane ni maadui wa Muungano,"
alisema Dk. Slaa.
Alisema
inasikitisha kuona kuwa kuna baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar ndani ya
Bunge hilo wakidanganywa kuahidiwa kupewa fedha za kuwasomesha ili
waunge mkono msimamo wa kupiga kura ya serikali mbili jambo ambalo ni
kinyume cha malengo ya uwakilishi wao kwa Watanzania.
"Chini ya
Umoja wao wa Ukawa wanachofanya ni kutetea maoni ya wananchi
yaliyotolewa kwenye Tume ya Katiba kwa kuwa Tanzania ni nchi ya wote na
hakuna, ambaye akifa atazikwa nje ya nchi hii. Hivyo, ni lazima kutetea
maslahi ya wananchi," alisema Dk. Slaa.
KAIMU KATIBU MKUU WA CUF ANENAKaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, alisema Tume ya Maridhiano ya Zanzibar inayoundwa na viongozi kutoka CCM na CUF ikiongozwa na Nassoro Moyo, imetoa tamko la kumtaka Rais asidhani Watanzania ni watu wa kuhadaiwa, bali watatetea serikali tatu kwa kuwa ina lengo la kuimarisha Muungano uliopo.
SIASA, KITAIFA, KIMATAIFA, MICHEZO,
KIMATAIFA MICHEZO,
KITAIFA,
SIASA
Location:
East Africa
Subscribe to:
Posts (Atom)