Israel
imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na
baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika
ukanda wa Gaza.
Katika
kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili
wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na
Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka
Gaza.(MM)
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa
miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia
Israel.