Israel
imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na
baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika
ukanda wa Gaza.
Katika
kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili
wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na
Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka
Gaza.(MM)
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa
miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia
Israel.
Vifaru
karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani
na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda
hata hospitali zimegwa na mizinga.
Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.
Kundi la
Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema
Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.
Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.
Jana
jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na
usitishwaji mapigano wa kudumu baada pande zote mbili kukubali
mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za
kibinadamu.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment