Thursday, July 17, 2014

Shule 10 bora 2013 zaporomo

Shule ya Sekondari Kisirimi iliyopo Wilayani Arumeru mkaoni Arusha  
Na Mussa Juma, Mwananchi
Kwa ufupi

Kismiri (pichani) imeshika nafasi ya tatu kati ya shule 10 bora nchini mwaka huu, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
SHARE THIS STORY
0
Share


Arumeru. Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kisirimi wilayani Arumeru, Arusha, Emmanuel Kisongo amesema kufanya vizuri kwa shule yake ni kuthibitisha shule za kata zinaweza kuwa bora nchini.
Kismiri (pichani) imeshika nafasi ya tatu kati ya shule 10 bora nchini mwaka huu, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Akizungumza na Mwananchi jana, Mwalimu Kisongo alisema mwaka huu wanafunzi wa shule yake wamefanya mtihani wa kidato cha sita kwa mara ya saba na shule imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa mara ya kwanza.
“Nimefurahi tumeingia kwenye shule 10 bora nchini mara tano na safari hii tumeshika nafasi ya tatu. Ni wazi shule za kata zinaweza, tofauti na fikra za wengi kuwa shule zipo chini kielimu,” alisema.
Kisongo alisema mwaka jana walishika nafasi ya tano, kitaifa na mwaka juzi, walishika nafasi ya tatu kama mwaka huu.
“Siri ya mafanikio yetu ni ufundishaji mzuri na ushirikiano mzuri wa walimu, wanafunzi na wazazi kwa lengo kubwa la kuthibitisha kuwa walioanzisha shule ya kata hawakufanya makosa,” alisema.
Alisema shule yake, ambayo ina jumla ya walimu 32 kati yao 12 wanafundisha kidato cha tano na sita, inafuata michepuo ya sayansi na sanaa (art) na mwaka huu wanafunzi 52 walifanya mtihani.
“Tunajivunia mafanikio haya na malengo yetu kuifanya shule hii kuwa bora nchini kwani ipo katika mazingira tulivu na wanafunzi wa dini zote tunawajenga kuwa na hofu ya Mungu,” alisema.
Alisema kwa sasa wanafunzi wa shule hiyo, wanajitambua na wanaheshimu masomo yao. Hawana muda wa migogoro na shule, jambo ambalo linawapa muda mzuri kusoma.
Shule 10 bora 2013 zaporomoka
Ibrahim Yamola, Mwananchi
Dar es Salaam. Shule za sekondari zilizokuwa kwenye orodha ya Kumi Bora ya matokeo ya kidato cha sita mwaka jana zimeporomoka, huku shule isiyo maarufu ya Igowole, mkoa wa Iringa ikichomoza kutoka nafasi ya nane hadi ya kwanza mwaka huu

ka

No comments:

Post a Comment