Wednesday, December 28, 2016

Polisi Morogoro wawashikilia watuhumiwa 12 Watuhuniwa waliomchoma Mkuki Pius

Jeshi la Polisi mkoa wa morogoro linawashikilia watu kumi na wawili kwa tuhuma za kumjeruhi na kumchoma mdomomi mkuki uliotokezea shingoni Augustino Pius mkazi wa kijiji cha Dodoma Isanga wilayani kilosa ambapo saba kati yao tayari wamekifishwa mahakamani.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa morogoro Ulrich Matei amesema kuwa wafugaji jamii ya kimasai wilayani kilosa mkoani morogoro waliwashambulia wakulima kwa silaha za jadi na kuwajeruhi watu sita mara baada ya kukamatwa kwa mifugo ilioyokuwa inaharibu mazao shambani.

Wakati huo naibu katibu wa chama cha wafugaji Tanzania Joshua Lugaso amesema kitendo cha mfugaji kumchoma mkuki Augustino Pius kinalaaniwa vikali na uongozi wa wafugaji na wafugaji wenyewe huku akivitaka vyombo vya sheria kuchukua hatua dhidi ya wahusika

No comments:

Post a Comment