Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia sabuni
inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'. Sabuni hizo zinadaiwa
kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa
kushiriki tendo la ngono na mwanaume.
Baadhi ya wasichana waliohijiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia
sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha
hali ya ubikira. Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka
nchini Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine
kwenye uke ni hatari.
Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani.(bbc)
No comments:
Post a Comment