eshi
la Polisi linawahoji watu nane wakiwemo Madaktari wa chuo cha kitabibu
cha IMTU kwa madai ya kutupa mabaki ya masalia ya binadamu katika msitu
mdogo uliopo eneo la Mpiji kata ya Mbweni wilayani Kinondoni Dar es
salaam.
Kamanda
wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema
kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova
‘Kuharibika kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea kuitengeneza’ – Aminiel
CHNAZO. MILLARD
No comments:
Post a Comment