Sanamu: Phil Neville amsema Wayne Rooney anaweza kufanikiwa kujengewa sanamu kama ataendelea kufanya makubwa.
PHIL Neville amedai kuwa Wayne Rooney
anaweza kuwa gwiji wa Manchester United na hata kupata heshima ya
kujengewa sanamu katika klabu hiyo.
Beki huyo wa zamani wa United aliyasema
hayo wakati anazungumzia nahodha mpya wa klabu na alidai kama mchezaji
huyo wa zamani wa Everton anataka, anaweza kuingia katika orodha ya
wachezaji wakubwa zaidi waliowahi kutokea katika historia ya klabu.
"Kama unavunja rekodi ya Bobby Charlton katika klabu ya Manchester United, unazungumzia heshima ya sanamu," Neville aliwaambia The Mirror.
"Kwasababu amekuwa mchezaji mkubwa kwa
wakati wote. Watu wanampenda Wayne Rooney, ninaposema anastahili sanamu,
namaanisha kuwa ni mchezaji mkubwa.
Mafanikio: Wayne Rooney ameshinda makombe matano ya ligi kuu tangu alipojiunga na Manchester United
No comments:
Post a Comment