Lori la mafuta baada ya kuanguka.
Lori la mafuta baada ya kuanguka.
Foleni iliyosababishwa na ajali hiyo eneo la Kimara, Dar.
Polisi wakidumisha ulinzi eneo la ajali.
Na Gabriel Ng’osha/GPLGARI lenye namba T748 ABJ lililokuwa limebeba mafuta ya diseli kutoka Dar es Salaam kwenda Singida, limeanguka leo asubuhi na kusababisha foleni ndefu maeneo ya Kimara-Darajani jijini Dar es Salaam.
Dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja la Juma, alikimbizwa hospitali. Gari hilo lilikuwa na lita 34,000 za mafuta, mali ya Nassor Filling Station ya jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo wananchi wa maeneo hayo, badala ya kutoa msaada, walianza kuiba mafuta hayo kabla ya kutawanywa na polisi waliofyatua mabomu ya kutoa machozi na juhudi za kulitoa barabarani zikaanza mara moja.
No comments:
Post a Comment