NMB katika kuongeza idadi ya matawi yake na kuhakikisha inawafikia
watanzania wengi na kila kona nchini, jana imezindua tawi jipya la
wilaya mpya ya Nanyumbu katika mkoa wa Mtwara.
Kwa sasa NMB imefikisha matawi Zaidi ya 150 na wateja Zaidi ya milioni 2
huku ikijivunia ATM mashine Zaidi ya 500 nchi nzima. Hiyo ni idadi
kubwa kuliko benki yoyote Tanzania.
Ufunguzi wa tawi hili ni Faraja kubwa kwa wakazi wa Nanyumbu ambao
wamekuwa wakipata tabu kufuata huduma za kibenki wilayani Masasi. Uwepo
wa NMB pia utarahisisha biashara kwa wakazi wa Nanyumbu kwani wengi wao
wanafanya biashara na wananchi wa Msumbiji. Ubadirishaji wa
fedha za kigeni pia ni mojawapo ya huduma itakayosaidia wakazi wa Nanyumbu nan chi ya Msumbiji.
NMB pia ili kusogeza huduma Zaidi kwa watanzania, measisi ubunifu mkubwa
katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya
simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM.
NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa,
masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na
biashara. Lakini Pia imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo
na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani
kupitia vyama vya ushirika nchini.
No comments:
Post a Comment