Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel
Sitta akizungumza na wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini
walipomtembelea ofisini kwake Dodoma jana. Wafugaji hao walipelekwa
bungeni hapo na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa
Magharibi, John Shibuda (kushoto). Picha na Emmanuel Herman
Mwenyekiti
wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema mikutano ya Bunge hilo haiwezi
kusitishwa na kwamba itaendelea kwa kuwa idadi ya wajumbe waliopo
inakidhi matakwa ya kisheria kutunga Katiba.
Kadhalika
Sitta amewatuhumu wajumbe wa wanatokana na kundi la Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kwamba si wazalendo kutokana na kususia Bunge hilo
tangu Aprili 25, mwaka huu.(Imakulata Ng'elenge)
Akizungumza
na wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini walioongozwa na Mbunge wa
Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda waliopeleka
mapendekezo
yao ili yaingizwe kwenye rasimu ya Katiba, Sitta alisema wanaotaka
Bunge hilo liahirishwe ni watu wasiolitakia mema Taifa.
"Lakini
napenda kuwaambia kuwa Bunge la Katiba liko hapa kisheria kwa kanuni
zake linaendelea na wale wanaopiga kelele lisiendelee ni watu ambao
hawatutakii mema," alisema Sitta na kuongeza;
"Kwa
sababu demokrasia yoyote ni kupata kura za wengi, walioko hapa wanatosha
kabisa kuendelea na mchakato huu mpaka mwisho wake kwa sababu tunaamini
wakati wa Katiba Mpya umefika."
Kauli ya
Sitta imekuja siku moja tangu viongozi wa Ukawa unaojumuisha vyama vya
NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF watangaze kwamba wataitisha maandamano nchi
nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge hilo kwa maelezo kwamba ni
matumizi mabaya ya fedha za umma iwapo Bunge hilo halitasitishwa.
Kadhalika,
baadhi ya wabunge wa CCM wamesikika wakitaka Bunge hilo liahirishwe ili
kunusuru fedha zinazotumika kugharamia shughuli zake, kwani hakuna
uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili ya kuwezesha Katiba hiyo
kupatikana.
Sitta
alisema hakuna ubishi kwamba baadhi ya wajumbe walitoka ndani ya bunge
hilo na kwenda nje ambapo wamekuwa wakipiga kelele na kwamba wao
(waliobaki bungeni) ambao wana uzalendo lazima wahangaike nayo mpaka
iweze kupatikana.
Alisema upungufu uliopo katika Katiba ya sasa, ndiyo unaofanya kutotungwa kwa sheria bora ambazo zitawezesha maslahi ya makundi mbalimbali yapatikane bila kuleta migongano kama iliyopo sasa.
"Ndio
maana sisi tunasema kung'ang'ania suala la muundo wa serikali ni kwenda
pembeni kidogo na matarajio ya watu. Huu ni ushahidi dhahiri kabisa kuwa
lililo muhimu ni haki za raia," alisema.
Alisema
hata kama Katiba itakuwa na muundo wa serikali kwa idadi yoyote, ikiwa
haitazingatia haki za makundi kama wafugaji, haitakuwa na maana
No comments:
Post a Comment