Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kila mwaka kwenye viwanja
vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wakati
alipotembelea na kukagua mabanda ya makampuni mbalimbali yanayoshiriki
kwenye maonyesho hayo
Rais Jakaya Kikwete akielekea ofisini kwa ajili ya kusaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa TANTRADE leo, katikati ni Dr. Abdallah Kigoda
Waziri wa Viwanda na Biashara na kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje
TANTRADE Bi. Anna Bulondo 
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Ofisa Mauzo Mwaandamizi wa kampuni
ya Gold Finger Investiment Bi.Beatrice Kibanya wakati alipoteaembelea
banda hilo. 
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. Edwin Wekefield wa kampuni ya
Mimic Craftis kutoka nchini Afrika kusini inayojishughulisha na masuala
ya mawasiliano. 
Mshauri wa jeshi la Magereza Bw. Alferio akitoa maelezo kwa Rais
jakaya Kikwete kuhusu kofia bora za kujikinga waendesha pikipiki wakati
alipotembelea katika banda la Mafereza 
Rais jakaya Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo
ya nje wakati alipotembelea katika banda hilo leo Mh. Rais Jakya Kikwete
aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa
Kimataifa. 
Rais jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa
Mawasliano wa Umoja wa Mataifa (UN)wakati alipotembelea banda hilo leo
na kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo
hapa nchini.
Rais
jakaya Kikwete akizungumza na vijana waliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa
katika mafunzo ya ujasiriamali wa tatu kutoka kulia nji Bi Hoyce Temu
Mtaalamu wa Mawasiliano wa umoja wa Mataifa (UN)
Rais jakaya Kikwete akimsalimia mtoto ambaye jina lake halikufahamika
mara moja wakati akitembelea katika mabanda mbalimbali kwenye viwanja
vya Sabasaba leo
No comments:
Post a Comment