Saturday, May 31, 2014

MWANAFUNZI WA TUMAINI- IRINGA ASHINDA TV YA COCA-COLA.

MSHINDI_7_19eee.jpg
MSHINDI_8_b230b.jpg
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Iringa, Vincent Lugendo (katikati) akifurahia Tv.

MSHINDI_10_87e29.jpg
Mkazi wa Frelimo A, Mzee Mahmoud Juma Tagalile, 64 akielezea jinsi alivyopata bahati ya kushinda TV kwa MC 

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini- Iringa, kitivo cha sheria, Vincent Lugendo ameshinda TV katika shindano la Coca–Cola la Jionee Mwenyewe Kombe la FIFA la Dunia mwaka 2014, alikuwepo pia Mzee Mahmoud Juma Tagalile, 64 mkazi wa Frelimo A, Manispaa ya Iringa, imefahamika.
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza leo imekabidhi zawadi ya luninga mpya aina ya Sony BRAVIA FIFA WORLD CUP 32, FIFA OFFICIAL TV, kwa washindi 14 wa shindano la Coca-Cola la Jionee Mwenyewe Kombe la FIFA la Dunia, mkoani Iringa.
Akikabidhi zawadi hizo, Afisa Mauzo na Masoko Nyanda za Juu Kusini/kati (Iringa, Njombe na Ruvuma), Mrisho Ramadhani alitoa rai kwa Watanzania kushiriki shindano ambalo zawadi yake ya juu ni tiketi za kwenda nchini Brazil kushuhudia mchezo wa robo fainali wa Kombe la FIFA la Dunia. Zawadi nyingine ni televisheni, mipira maalumu ya Kombe la Dunia na fulana.
MSHINDI_20_e44be.jpg
Akabidhi zawadi kwa washindi 14 wa mkoa wa Iringa katika Stendi Kuu ya mabasi yaendao mikoni leo mchana, afisa mauzo na masoko huyo aliwaomba wananchi kushiriki mara kwa mara ili kupanua wigo wa kujishindia zawadi mbalimbali.
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi zao, washindi wote walionesha kuzifurahia na kusema kuwa shindano hilo ni halisi na kwamba kila mtu anaweza kuibuka mshindi, ambapo kila mmoja wa alikabidhiwa TV inchi 32 yenye thamani ya shilingi 900,000/- (sawa na shilingi 12,600000/- kwa TV 14).
Washindi wanapatikana kwa kunywa soda ya chupa ya Coca- Cola na kupata vizibo viwili vyenye kutengeneza neno Brazil pamoja na kizibo cha ushindi.
Kizibo cha ushindi kina picha ya kitu ambacho mteja ameshinda (Tv, Mpira au T-shirt) wakati kizibo cha ushindi wa zawadi ya tiketi kina nembo ya ndege.
Kampuni ya Coca-Cola ni mshirika wa Fifa kwa muda mrefu, ambapo uhusiano rasmi ulianza tangu 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa michuano ya Kombe la Dunia 1978. Coca-Cola imekuwa na matangazo kwenye viwanja vinavyochezewa michuano ya Kombe la Dunia tangu 1950

No comments:

Post a Comment