Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (kushoto)
akipokea hati ya makubaliano kutoka kwa Mkurugenzi wa TPB Bw Sabasaba
Moshingi (kulia) katikati ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo
Bw Juma Nkamia wakati wa Uzinduzi wa Kadi Mpya za ATM za Wanachama
Shirika la Benki ya Postay nchini (TPB) na klabu ya Young Africans leo
wamezindua rasmi kadi mpya za wanachama zenye mfumo wa Kielektoniki
(ATM) ambazo zitaanza kutumika mwezi Juni mwaka huu kwenye sherehe
zilizofanyika katlika Hoteli ya Hyatt (Zamani Kempsink) eneo la Posta
jijini Dar es salaam.
Sherehe hizo za uzinduzi wa kadi mpya za wanachama zilifanya na mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Bw Juma Nkamia ambaye
aliipongeza Benki ya Posta na vilabu vya Simba na Yanga kwa hatua nzuri
waliofikia ya kisasa ya kuongeza wanachama na kujikomboa kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta nchini Bw Sabasaba Moshingi
alisema wao kama Benki ya kizalendo wameamua kuanza na vilabu viwili
vyenye wapenzi na wanchama wengi kwa ajili ya kuvisaidia kuwafikia watu
wao nchini kote na kongeza pato la vilabu vyao kwa kulipia ada zao
kupitia Benki ya Posta.
"Benki yetu ina matawi nchini kote, hivyo kwa sasa watu wanaopenda kuwa
wanachama wa Yanga na walikua wanashindwa kufika makao makuu kupata kadi
zao, njia imekua rahisi wanaweza fika kwenye matawi yetu nchi nzima na
wakajiandaikisha kisha baadae kupewa kadi zao za uanachama zenye mfumo
wa ATM ambazo pia wataweza kuzitumia katika shuguli zingine za Kibenki,
kuweka, kutoa kwenye mashine za Umoja Switch nchi nzima" alisema
Sabasaba.
Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw Clement Sanga
alisema wanaishukuru Benki ya Posta kwa kukubali kufanya kazi hiyo ya
kuandikisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kisasa
jambo ambalo litapelekea kuongeza idadi ya wanachama kwa urahisi na
kuongeza pato la klabu.
Aidha Sanga alisema kwa mfumo huu mpya ni rahisi kujua wanachama walio
hai kwa kuwa kutakua na kumbukumbu zote kwenye mtandao ambapo
wamanachama asiye hai kadi yake haitakua na uwezo wa kusoma kwenye
mashine wala kupata huduma zozote za Kibenki.
No comments:
Post a Comment