Msanii wa Bongo Fleva AY akiwa amewasili na crew yake nzima kuja
kumpa pole Mbonie Masimba, AY alitoa laki 6 kununua jeneza la marehemu
Tyson hii ikiwa kama mchango wake kwa kuthamini kile alichomfania wakati
akiwa hai. Sasa msafara unaelekea Bongo na mwili utafikia Hospital ya
Kairuki iliyopo Mikocheni na naambiwa msiba uko upo Bahari Beach
nyumbani kwa marehemu.PICHA ZAIDI HAPA
Wasanii na watu mbalimbali waliofika kuaga mwili wa George Tyson
aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari Morogoro baada ya
gari alilokuwa akiendesha marehemu kuacha njia na kupinduka huku
likibingilika mara tatu ndani ya gari hilo pamoja na abiria wengine
kuwepo kiti cha nyuma alikuwemo MC maarufu Gladys Chiduo maarufu kwa
jina la MC Zipopamba aliyekuwa amekaa kiti cha mbele na amesema
kilichomuokoa yeye ni kufunga mkanda.
Wasanii na watu mbalimbali wakiwa kwenye mstari wa kuaga mwili wa marehemu George Tyson.
Picha kwa hisani ya Dj Choka Blog
No comments:
Post a Comment