Nyama ya mbuzi mbavu na inawekewa marination ya kawaida tu ili kuilainisha na kuipa ladha kabla ya kuichoma. Tunatumia tangawizi,kitunguu saumu,ndimu au limao na chumvi.Nyama
inapakwa hivyo vyote kisha inawekwa kwenye fridge kama lisaa hivi ndio
inaanza kuchomwa.Inaweza kuwekwa hivyo vyote hata usiku ikalala kwenye
fridge kesho yake ikachomwa.
Kuku
nao huwekwa marination ila hii ni kitunguu saumu na limao na
chumvi.Wakati mwingine tunaweza kufanya chicken tandoor kama tunataka
ile ladha ya pilipili.
Hii ni mbuzi ikiiva taratibu….
Mambo yako tayari kuliwa..
LUNCH:Mbuzi choma,ugali,kachumbari na mboga ya majani ya maboga.
DINNER:Kuku choma,ndizi tamu za kukaaanga na kachumbari bila kusahau chachandu.
No comments:
Post a Comment