Hatimaye kimeleeweka, hivi ndivyo utakavyoweza kutamka baada ya uongozi
wa Yanga kuwalipa wachezaji wake mshahara na posho zao za mechi za Ligi
Kuu Bara walizocheza.
Hiyo imekuja siku chache baada ya wachezaji hao kugomea mazoezi ya timu
hiyo kwa siku mbili mfululizo, wakidai mshahara wa Novemba, mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, wachezaji hao walilipwa mshahara na posho hizo juzi Ijumaa.
“Hakuna mchezaji yeyote anayeidai Yanga, kwa kifupi wachezaji wote
wamelipwa mishahara sambamba na posho za mechi mbili walizokuwa
wanazidai.
“Kikubwa kilichokwamisha wachezaji kulipwa kwa wakati ni mfumo
uliobadilika katika malipo hayo, lakini kila kitu kilikuwa kipo vizuri,
hivyo wachezaji wanachotakiwa hivi sasa ni kufanya kazi yao ndani ya
uwanja.
“Kama uongozi tumejipanga vema kuhakikisha kuwa tatizo hili
lililojitokeza halitajitokeza tena kwenye timu yetu, hivyo tumeandaa
utaratibu mzuri wa malipo hayo,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, kuzungumzia hilo,
alisema: “Kila kitu kipo vizuri kwenye timu, kwa maana ya malipo ya
mshahara wao wa mwezi Novemba ambao wamelipwa.
“Hivyo, hakuna mchezaji yeyote anayedai mshahara katika timu na kitu
kikubwa kilichobaki ni wachezaji kutimiza majukumu yao ya uwanjani.”
Nahodha Mkuu wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro', alilithibitisha
hilo kwa kusema: “Hakuna mchezaji anayedai mshahara katika timu,
wachezaji wote tumelipwa mshahara wetu wa mwezi Novemba
No comments:
Post a Comment