Meneja
mradi wa ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Mhandisi Mwanaidi Mkwizu (aliyevaa suti) akitoa melezo kwa Timu
ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango.
Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeo ikiendelea na ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo ndani ya jengo la abiria.
Mwonekano wa sehemu ya mbele wa Jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal III).
Na Adili Mhina, DSM.
Tume
ya mipango imefanya ziara katika mradi wa ujenzi wa jengo la III la
abiria katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (Terminal III) jijini
Dar es Salaam kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi huo na kuelezwa
kuwa ujenzi umefikia asilimia 65.
Akitoa
maelezo mbele ya timu ya wataalamu kutoka Tume ya Mipango, Meneja wa
Mradi huo Mhandisi Mwanaidi Mkwizu alieleza kuwa ujenzi
huo unaotekelezwa na Mkandarasi wa kampuni ya BAM kutoka Uholanzi
ulioanza Juni 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba Mwaka
2017.
Akielezea
miundombinu ya uwanja huo, Mhandisi Mkwizu alisema kuwa uwanja huo wa
kisasa una barabara ya kuruka ndege (runway) yenye urefu wa kilometa 3
na upana wa mita 60 ambapo upana unaohitajika kwa matumizi ya ndege ni
mita 45.
Aliongeza
kuwa mradi huo pia umeangalia changamoto ya kukatika umeme mara kwa
mara na kuamua kutafua vyanzo mbalimbali ili kuondokana na utegemezi wa
chanzo kimoja ambacho kinaweza kukwamisha shughuli katika uwanja huo
pale inapotokea hitilafu.
Alieleza
kuwa kutakuwa na njia mbili tofauti za kuleta umeme kutoka TANESCO
ambapo njia moja ni kwa ajili ya dharura na pia endapo kutakuwa na
tatizo la kukatika umeme kupitia njia za TANESCO, umeme utapatikana
kutoka chanzo mbadala cha dharura kwa kutumia jenerata nne kubwa za
kisasa za dizeli zilizopo eneo la mradi ambazo zinatosha kukidhi
mahitaji ya eneo hilo.
Alisisitiza
kuwa tayari wamefanya mazungumzo na TANESCO na kukubaliana kuwa njia
hizo za umeme ni kwa ajili ya uwanja huo pekee na hakuna wateja wengine
watakaounganishiwa katika njia hizo.
Mhandisi
mkwizu alimalizia kwa kusema kuwa yeye pamoja na timu yake ya wataalamu
wanaendelea kufanya usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na malengo yaliyopangwa.
Wataalamu
wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango walipata fursa ya
kutembelea maeneo mbalimbali ya ujenzi wa mradi huo na kuonesha
kuridhishwa na kasi yautekelezaji huku wakimshauri menejea wa mradi huo
kuendelea na ufanisi wake katika kusimamia kazi hiyo ili kuhakikisha
malengo ya mradi huo yanafikiwa.
Eneo watakapopita abiria kutoka ndani ya jengo la abiria wakielekea kupanda ndege.
Moja ya sehemu za ndani ya jengo la abiria.
Sehemu ya ujenzi unaoendelea katika mradi huo.
Mhandisi
Omari Athuman (mwenye kofia ya bluu) akiangalia kazi ya kuunganisha
mitambo ya moja ya majenereta ya kisasa kwa ajili ya dharura ya umeme
katika uwanja huo.
Majenereta ya kisasa kwa ajili ya dharura ya umeme katika kiwanja hicho.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha kisasa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Mwanaidi Mkwizu (wa
kwanza kushoto) akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi huo mbele ya timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango pamoja na
wajumbe kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati wa ziara
ya ukaguzi wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment