Sunday, August 10, 2014

WAPO WALIOFUNGA NA WAPO WALIOSHINDA NJAA MWEZI WA RAMADHANI...

Na Mathias Canal, Kwanza Jamii-Iringa
Kufunga kunahitaji kujitoa hakika ili kupata thawabu kwa mwenyezi mungu lakini wapo waliofunga kwa shinikizo la wenza, dini, rafiki, ndugu na hata jamaa zao wa karibu.
Lengo la kufunga wakati mwingine ni kuondoa na kuzuia tama zote unazokuwa nazo
1. kufunga ni Amri: (umma wa nabii Musa na Issa, wao walikua wanafunga kila mwezi siku tatu na siku ya Ashura (inajulikana kama Pass ver au Pasakha) lakini wanaofunga sasa walipunguziwa siku.
2. kufunga kunafuta Madhambi (Mizigo). Mungu amesema katika sura#33 aya#35. Ukijaaliwa pata thawabu, itafute uisome, I have run out of space.
Mke wa mtume (s.a.w) Ummu Salama, alimuuliza Mtume "wamaume mnatajwa kwenye Qurani sisi Je? Siku ile ile saa za Adhuhuri aya hii ikashuka.

(Dalili ya Muslima activism)
Nawapongeza wale waliofunga kwa kumaanisha lakini nawapa pole wale waliofunga njaa na wanajitambua kabisa kuwa walishinda njaa kisa dhambi wazifanyazo kwa kujua au kutojua.Hakika kwa macho yangu mawili nilimshuhudia kijana mmoja akiwazulumu watu huku akijinadi kwa kufunga njaa ila wengine tulimtazama kwa kuamini alishinda njaa.
Mungu awe mwema kwetu na kutambua thamani ya binadamu wengine ukizulumu milioni au laki moja mie naanza kukutazama utafanya nini cha maana kama sio kufanyia starehe, maana wapo wale ambao wakiwa si walevi basi watavuta sigara, na wasipofanya yote hayo basi watajihusisha na ngono zembe(wapenzi wengi) huku wakijikinga na mwamvuli wa dini. Lakini wapo ambao ni wacha mungu hakika

No comments:

Post a Comment