Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka
akipokewa na Felic Maagi Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakati alipowasili
kwenye Banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere
barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka
akizungumza na baadhi ya viongozi wa shirika la nyumba nchini NHC baada
ya kuwasili kwenye banda hilo tayari kwa kukagua shughuli zinazofaywa na
shirika hilo, Kutoka kulia ni Muungano Saguya Meneja za Jamii NHC,David
Shambwe Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa NHC .(PICHA NA
KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijjuka
akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo wakati alipotembele
banda la NHC Kushoto ni Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha na kutoka kulia
ni Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa
Mawasiliano NHC. 
Mmoja wa watu waliotembelea banda la NHC akipata maelezo kutoka kwa
maofisa wa shirika hilo kutoka kulia ni Nalindwa Norbert, Rhobi Wambura
na Wilson Sanane. 
David Shambwe Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa NHC akitoa
maelezo wa Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna
Tibaijuka wakati alipotembelea banda la shirika hilo kushoto ni Felix
Maagi Mkurugenzi wa Fedha na Kutoka kulia ni Rhobi Wambura na Wilson
Sanane maofisa wa NHC. 
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika bana hilo. 
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka
akzungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda hilo kushoto
ni Bw. Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha NHC.
1.Nalipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri wanayofanya ya
kuwapatia wananchi makazi bora. Sisi upande wa Serikali tutaendelea
kuwasaidia kisera ili waweze kutimiza wajibu wao vizuri zaidi. 2. Pamoja
na ujenzi wa nyumba wanaoufanya katika maeneo mbalimbali nchini na kwa
watu wa vipato vya chini na watu wa vipato vya kati na juu, Serikali
inaupongeza mpango wa Shirika waliouanza kwa kasi wa kujenga nyumba za
gharama nafuu nchini, mpango unaoendeshwa kwa kaulimbiu ya “nyumba
yangu, maisha yangu” 3. Nyumba hizo sasa zimekamilika katika maeneo 14
ya Halmashauri za miji ikiwemo Mkinga(Tanga), Mvomero(Morogoro),
Mnyakongo-Kongwa(Dodoma), Mkuzo (Songea), Mtanda(Lindi), Mrara(Babati),
Unyankumi(Singida), Kibada na Mwongozo (Kigamboni), Bombambili(Geita),
Ilembo na Inyonga(Katavi), Uyui(Tabora), Longido na Monduli(Arusha) na
Mlole(Kigoma). Miradi mingine ya aina hii imeanza kutekelezwa katika
Halmashauri mbalimbali za Miji na Wilaya hapa nchini, lengo likiwa ni
kufikia Mikoa yote na ikibidi kila Halmashauri nchini. 4. Ili kuufanya
mpango huu mzuri wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kuwa endelevu,
mambo kadhaa ni lazima yafanyike:- Kwanza ni kwa Halmashauri kote nchini
kuunga mkono kwa kulipatia Shirika maeneo ya kujenga nyumba hizo
yasiyokuwa na masharti magumu. Ardhi isifanywe kitegauchumi na
Halmashauri kwa kuiuza kwa gharama kubwa kwani kufanya hivyo kutafanya
nyumba zinazojengwa kuwa aghali. Pili, Halmashauri na wananchi kwa
ujumla wajitokeze kwa wingi kununua nyumba zinazojengwa na NHC ili
mapato yatakayopatikana yawezeshe kujenga nyumba zingine kwa ajili ya
wananchi. 5 Zipo pia nyumba zinazojengwa katika miji mikubwa “satellite
cities” zenye lengo la kuwapatia wananchi makazi na kuondoa msongamano
wa magari mijini. Miji hiyo ni pamoja na Burka, Usar River na Mateves
Arusha, Luguruni, Kunduchi Rifle Range,
Uvumba na Kawe - Dar es salaam. Aidha, katika mikoa kadhaa hivi sasa
majengo makubwa ya biashara yanajengwa ili kuipa sura mpya miji yetu na
kukuza shughuli za kibiashara. 6. Serikali inaitambua sekta ya nyumba
kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na
kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, nalihimiza Shirika hili
liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili
kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Wananchi wengi wakimiliki
nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana
wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya
kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. 7. Nawasihi watanzania watembelee
banda hili la NHC ili wapate taarifa za kina za namna ya kununua nyumba
na mahali nyumba hizo zilipo
No comments:
Post a Comment