Muhubiri wa kiisilamu ameuawa mjini mombasa pwani ya Kenya , ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni ya kiongozi mwingine wa kidini.
Sheikh
Mohammed Idris, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri
nchini Kenya, aliuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumba yake na
watu wasiojulikana.
Duru
zinasema kwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi
kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake.
Wahubiri kadhaa mashuhuri wameuawa katika hali ya kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.
Wengine
waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo
la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa mauaji yao, madai
ambayo serikali imakenusha.
Marahemu
Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye
itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi
ya waumini kumuita msaliti.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment