
Ugonjwa
wa saratani unazidi kushika kasi kila kukicha hapa nchini. Pia
umegharimu maisha ya watu wengi kutokana na huo ugonjwa bado haujapatiwa
tiba madhubuti.
Mbali na
kugharimu maisha ya watu wengi, ugonjwa huu umekuwa tishio kutokana na
gharama kubwa za matibabu zinazowagharimu wagonjwa.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa Februari wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Saratani Dunia, takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi
zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, zenye ongezeko kubwa la wagonjwa wa
saratani.(Martha Magessa)
Takwimu
hizo zinaeleza kuwa kila mwaka wagonjwa wapya 21,180 hugundulika. Aidha
zaidi ya watu 16,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.
Kati ya wagonjwa 40,000 wanaokwenda kutibiwa kwenye hospitali maalumu,
asilimia 80 ya wagonjwa hao wanafariki dunia kutokana na maradhi ya
saratani.
Licha ya
ugonjwa huo kugharimu maisha ya watu wengi, baadhi ya wagonjwa
wanaogundulika mapema, wataalamu wa afya huwashauri wafayiwe upasuaji
kwa lengo la kuondoa sehemu iliyoathirika na kuzuia usienee sehemu
zingine za mwili na kuleta madhara zaidi.
Hali hiyo
imemkuta kijana Gerard Mwambungu mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam,
ambaye ameamua kupiga magoti mbele ya Watanzania akiwaomba msaada wa
fedha ili aweze kupata matibabu na kunusuru maisha yake.
Mwambungu
ambaye hakuwahi kutegemea kama siku moja angekumbwa na maradhi hayo,
sasa nusura ya maisha yake iko mikononi kwa Watanzania.
Kijana
huyo amekuwa akisumbuliwa na saratani ya ngozi kwa muda wa takriban
miezi saba. Licha ya kwamba baada ya kuanza kuumwa hakufahamu kuwa
ingefika hatua ya kufanyiwa upasuaji.
Mwambungu
aliyekuwa mfanyabiashara wa viatu katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi
ya Mikoani cha Ubungo, baada ya kufanyiwa vipimo na wataalamu wa afya
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kugundulika na ugonjwa huo
kwenye mguu wake wa kulia sasa anatakiwa kufanyiwa upasuaji.
Chimbuko la ugonjwa huo
Mwambungu
anasema siku moja jioni baada ya mizunguko yake ya kutafuta riziki
alikuwa amejipumzisha sebuleni kwake. Akiwa hana hili wala lile,
akajisikia muwasho sehemu ya mguuni. Anasema kwanza aliinama na
kuangalia ule muwasho kama ni mkwaruzo alioupata akiwa kwenye mizunguko
ya siku ile au la.
Hata
hivyo Mwambungu anasema haukuwa mkwaruzo kama alivyodhania bali kilikuwa
ni kipele, kitu ambacho hakikumtia hofu, kwani haikuwa mara ya kwanza
kutokewa na kipele mwilini mwake, basi akajikuna usiku ukapita.
CHANZO:MWANANCH
No comments:
Post a Comment