Nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Ubungeni iliyokuwa ikishikiliwa
na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe itatangazwa baadaye Freeman
Mbowe,
Dodoma. Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ametangaza Baraza lake
la mawaziri kivuli 28 na naibu mawaziri 12, na kufanya baraza lote kuwa
na mawaziri 40.
Katika baraza hilo la mawaziri linalojumuisha wabunge wanaotokana na
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mawaziri 25 wanatoka Chadema, 11
wanatoka CUF na NCCR-Mageuzi ni wanne.
Mawaziri kivuli walioachwa katika baraza hilo ni Sylvester Kasulumbay
(Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Highness Kiwia (Viwanda na Biashara) na
Rose Kamili (Kilimo, Chakula na Ushirika).
Wengine walioachwa na Mbowe akasisitiza kuachwa kwao siyo kwa sababu
hawawezi kazi bali ni kutaka kuwa na baraza la mawaziri dogo ni Sabrina
Sunga (Naibu Waziri Maji).
Katika Baraza hilo, nafasi ya mnadhimu mkuu wa upinzani Bungeni
iliyokuwa ikishikiliwa na Tundu Lissu (Chadema) sasa itashikiliwa na
Mbunge wa Tumbe, Rashid Abdalah kutoka chama cha CUF.
Akitangaza baraza hilo Bungeni mjini Dodoma jana, Mbowe alisema Wizara
ya Katiba na Sheria imeongezewa majukumu ya Muungano na waziri wake
atakuwa ni Lissu na naibu wake ni Abdalah.
Pia amemteua Mbunge wa kuteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa
taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anakuwa Waziri wa Fedha
wakati Naibu wake atakuwa Christina Lissu kutoka Chadema.
Mawaziri Ofisi ya Rais ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Utawala
Bora-Chadema), Vicent Nyerere (Utumishi-Chadema) na Esther Matiko
(Mahusiano na Uratibu-Chadema).
Ofisi ya makamu wa Rais itakuwa na mawaziri wawili ambao ni mchungaji
Israel Natse kutoka Chadema atakayeshughulika na Mazingira na Naibu wake
atakuwa ni Assah Othman Hamad (CUF).
Mnadhimu wa Upinzani Bungeni ndiye atakayeshikilia pia nafasi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mazingira.
Mawaziri katika ofisi ya Waziri mkuu ni Pauline Gekul (Uwekezaji na
Uwezeshaji-Chadema), Rajabu Mohamed Mbaruku (Sera, Uratibu na Bunge-CUF)
na David Silinde (Tamisemi-Chadema).
Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika itashikiliwa na Meshack Opulukwa
(Chadema), Wizara ya Nishati na Madini atakuwa John Mnyika Chadema na
Naibu wake “atakuwa Raya Ibrahim (Chadema).
Kulingana na orodha hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa itashikiliwa na Ezekiah Wenje (Chadema) na Naibu wake ni
Rashid Abdalah kutoka CUF.
Mawaziri wengine na wizara zao kwenye mabano ni Felix Mkosamali
(Ujenzi-NCCR-Mageuzi), Magdalena Sakaya (Maji-Cuf), na Moses Machali
(Uchukuzi- NCCR- Mageuzi).
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaongozwa na Godbless Lema wa Chadema
na Naibu wake ni Khatibu Said Haji wa CUF wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Makazi ni Halima Mdee wa Chadema.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Mbowe amemteua Rose Kamili Sukum kutoka
Chadema kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakati Naibu wake
atakuwa ni Mkiwa Adam Kiwanga wa CUF.
Wizara ya Maliasili na Utalii itashikiliwa na mchungaji Peter Msigwa
(Chadema), Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeenda kwa Joseph
Selasini (Chadema) na naibu ni Rukia Ahmed Kassim (CUF).
Mbowe pia amemteua Masoud Abdalah Salim wa CUF kuwa Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa na Wizara ya Elimu itashikiliwa na Susan Lyimo
na Naibu wake ni Joshua Nasari wote toka Chadema.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeenda kwa Dk Gervas Mbassa na Naibu
wake ni Conchesta Rwamlaza wote wa Chadema. David Kafulila (NCCR)
ameteuliwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Katika baraza hilo la mawaziri, Injinia Habib Mnyaa wa CUF ameteuliwa
kuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakati Lucy Owenya
kutoka Chadema akiteuliwa kuwa naibu wake.
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imeenda kwa Baruan Salum Khalfan wa
CUF na Naibu wake ni Subreena Sungura wa Chadema. Cecilia Paresso wa
Chadema anakuwa Waziri wa Kazi na Ajira.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo imeendelea kushikiliwa na Joseph Mbilinyi wa Chadema.
Akizungumza na wanahabari, Mbowe alisema wakati katika Baraza la
Mawaziri la Serikali ya CCM, wanaume ni 36 na wanawake 15, wao upinzani
wanaume ni 26 na wanawake ni 14.
Hali kadhalika Mbowe alisema wakati Baraza zima la mawaziri la Serikali
ya CCM likiwa na mawaziri kamili 28 na manaibu 22, wao Baraza lao Kivuli
lina mawaziri kamili 28 na naibu mawaziri 12.
Alisema nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Ubungeni iliyokuwa
ikishikiliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe itantangazwa
baadaye
No comments:
Post a Comment