Paul C. Makonda Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
Leo Nitatumia maneno makali kidogo ili
tuelewane kiurahisi. Wapinzani wa Nchi hii ni “BAPHOON”. Maana ya
BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya Mataifa
Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata Kuchukua Mabomu na
kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)
Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.
Kwa tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi kusema;
“Power tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely. Great men are almost always bad men”
Yakimaanisha kuwa;
“Madaraka yana tabia ya kuwaharibu walio
nayo, na wenye madaraka makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata
watu wema hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka”
Na sisi Vijana Wazalendo tunasema;
“Watu wenye Madaraka Makubwa
Wakiharibiwa na hayo madaraka hulewa hayo madaraka na kuanza hata
kutukana kudharau waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa
wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na
wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona madaraka hayo ni
Mzigo wala si zawadi.”
Wapo wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani
vipo kwa ajili ya Maslahi ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani
ndio mkombozi wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa
hili ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani. Ukweli
halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa maslahi yao tu na
vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa
Taifa hili.
Hatuna haja ya kuwaambia BAVICHA waombe
radhi kwa matamshi yao yasiyo na adabu waliyoyatamka jana dhidi ya Rais
wa Jamhuri na Waziri Mkuu kwa sababu tunajua wanadhani wako sahihi.
Lakini tunajua wanajua hawako sahihi na wanafanya hivyo ili kuwaridhisha
mabwana zao ambao wanawatumia wao kutengeneza mitaji yao kisiasa. Wao
wanabaki tu kama kigenge fulani ambacho kama kikiachwa kikue na uwongo
wake mwishowe kitaaminiwa na hapana shaka nchi hii ipo siku itaongozwa
na Vichaa.
Tuelewe Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, ndiyo Lulu pekee iliyobaki Afrika ambayo imeundwa na sisi
wenyewe , kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake mbili
kutoka katika Ukoloni. Haiwezekani tuache Muungane uchezewe tu na
wachache wetu ambao kinachowasukuma ni Uroho tu wa madaraka.
Tulipoanzisha Mfumo wa Vyama vingi,
tulidhamiria kuwa na vyama vyenye nguvu za dhati ambazo ama zingekuwa
kubwa kuliko CCM ili kuweza kuiwajibisha serikali sawasawa nayo
iwajibike moja kwa moja kwa ujenzi wa taifa. Miaka 21 baada ya kuwa na
mfumo wa vyama vingi, tumekuwa na vyama legelege ambavyo havina dira
wala mwelekeo badala yake vimejikita katika uchochezi na ulaghai. Hali
hii inatupa wasiwasi kama kweli hivi ni vyama vya siasa ama ni vikundi
tu vya harakati vinavyofanya siasa. Watanzania wako tayari kuamini
Upinzani lakini si kwa miaka hii ya karibuni,ni mpaka tutakapopata vyama
vyenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya nchi hii huku vikithibitisha
kwamba vitadumisha muungano wa nchi mbili serikali mbili na kuheshimu
Katiba ya Nchi.
Chama Cha Mapinduzi kinabaki Imara na
Msimamo thabiti wa Kuendelea na Jamhuri Muungano wa nchi mbili na
Serikali Mbili. Azimio la kutaka serikali tatu si mara ya kwanza sasa.
Azimio kama hili lilikuwepo Mwaka 1993 kwa hoja Binafsi ya Wabunge 55
(G55) iliyopelekwa na Mh. Njelu Kasaka Mbunge wa Chunya. Kwa kikao Cha
Bunge cha August 24-27, Bunge liliridhia mchakato wa kuanzisha serikali
ya Tanganyika. Lakini kwa Uthabiti wa CCM ambao ni imara sana sasa
kuliko mwaka 1993, kilisimamia mfumo wa kubaki na Muungano wa Nchi mbili
na Serikali Mbili. Msimamo wa CCM wa Mwaka 1993 ni thabiti sana sasa,
hatuwezi kufufua Tanganyika isipokuwa tutatumia mfumo uliopo kutatua
kero za Muungano zilizopo. Changamoto kubwa zinazotukabili ni za
kiuchumi kuliko zilivyo za kijamii na muungano wetu sana una nia thabiti
ya kijamii kuliko uchumi.
Demokrasia imechukua njia hadi sasa hata
mifumo ya demokrasia imeanza kupuuzwa. Nasema inapuuzwa kwa sababu hata
Vichaa sasa wanaweza kuamka tu na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala
Miguu. BAVICHA ni Vijana wadogo sana ambao hawawezi kuamka na kutoa
matamko waliyoyatoa ila kwa kutumwa na Bwana zao. Na hao Bwana zao
wanafadhiliwa na Mataifa ya nje ambay hayataki kuona siku moja AFrika
inaungana na kuwa taifa moja kubwa. Namna pekee ya kufanikisha uovu huo
mkubwa dhidi ya Afrika, ni kuibomoa Tanzania, na wenzetu hawa wapinzani
wamekubali kutumika kama vibaraka wa kudidimiza Afrika.
Hatuoni Sababu ya Kukaa Kimya,
Sitanyamaza kufumbia macho Ujinga huu. Nani kawatuma BAVICHA kutoa
Matamko dhidi ya Rais na Waziri Mkuu? Nani kawadanganya kuwa eti
Mchakato wanaoutaka UKAWA ndio Mchakato wanaoutaka Wananchi?
Unamsikiliza Mh. Lipumba, amejawa maneno
kinywani mwake ya uchochezi tu wa kidini na ubaguzi wa wazi kabisa.
Hizo zote ni hila ambazo kama zisipodhibitiwa kwa kuelezwa ukweli wake
kama hivi, taifa litaangamia. Tumedhamiria kupambana na hili, hatutakaa
kimya Mpaka watanzania watuelewe na wawapuuze wapinzani kwa lugha zao za
uchochezi.
wa Nini wakatake kufanyia Mkutano
Zanzibar kibanda Maiti na Si Dodoma maana wote walikuwepo hapa? Hivi
wapi ni Karibu, Iramba kwa Tundu Lisu au Zanzibar (Unguja Kibanda
Maiti)? kuna Umbali gani Hai kwa Mbowe au Tabora kwa Lipumba au Vunjo
kwa Mbatia ukilinganisha na Zanzibar? Hawa waheshimiwa wasitake kulaghai
Umma, kuna ajenda wameibeba ambayo hawataki kuisema. Warudi Bungeni
waje wajenge hoja maana Katiba haitapatikana Majukwaani bali kwa
kukamilisha Mchakato Bungeni na ndicho CCM tutakachofanya. Tunaendelea
na Bunge na tunakamilisha Mchakato hata wasiporudi.
Ikiwa wao ni vyama vya kidemokrasia na
nia yao ni kujenga demokrasia, kwa nini hawataki kukaa meza ya
Mazungumzo? kwa nini wakimbie mkutano halali wa kidemokrasia wasikae
hapo wajenge hoja hapo badala yake wanakimbilia eti kwenye mikutano ya
hadhara? Hapo kuna walakini na demokrasia wanayohubiri. Anayehubiri
demokrasia lazima awe wa kwanza kukaa meza ya mazungumzo. Mumewasikia
wakitoa matamko kwamba hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na
serikali wala CCM, hawa ni washari na wanatangaza shari na kisha
wanatafuta huruma ya wananchi. Hiyo siyo demokrasia ni Vurugu. Uhuru
bila mipaka i vurugu na Demokrasia bila Utaratibu nayo ni vurugu.
Tunazo tetesi kuwa hivi vyama
vinafadhiliwa na wasiotaka kuiona Afrika ikiungana na kuwa jumuiya moja
kubwa yenye nguvu. wanatafuta ucku na Mchana kuisambaratisha Afrika na
namna pekee ye kuisambaratisha Afrika ni kuisambarataisha Tanzania kwa
maana Tanzania ndiyo kinara wa Umoja wa Afrika. Kutumiwa kwao na
Ukibaraka wao uendelee lakini tuko imara sana kulinda Muungano wetu.
Hawa ni BAPHOON.
Lugha za kichochezi za wapinzani
wananchi wamezisikia. Wamemsikia Prof. Ibrahim Lipumba akiweka matabaka
ya watu kwa sababu za Kidini, wamemsikia Tundu Lisu akipandikiza chuki
dhidi ya Mwalimu Nyerere na waasisi wa Muungano, Mumewasikia viongozi wa
CUF, NCCR Mageuzi, wakifanya juhudi za kufitinisha watanzania kwa kauli
zao ovu. Ufitini wa aina yoyote, uwe wa kidini, kikanda, kikabila au
haiba ya watu hauna budi kupigwa vita kubwa na kila Mtanzania mpenda
amani.
Wakumbuke, Chuki wanazozijenga sasa,
itafika mahali zitakomaa na zikishakomaa zitaanza kuwa mwiba mkali kwao
wao wenyewe. Kwa maana wakifanikiwa kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa
watanzania kwa namna yoyote ile, hakuna namna ambayo hao
waliowapandikiza chuki watawapenda wao. Chuki yao itawala wao wenyewe na
itaangamiza taifa. Hatuwezi kuacha hili litokee tukiangalia kwa macho
yetu.
Taifa halitajengwa na watu waoga wala
waongo na wafitini. Watanzania wenzangu tujikite katika kujenga uchumi
na kujiletea maendeleo kwani tukiendelea kuwasikiliza “BAPHOON” hawa na
kuacha shughuli zetu za kiuchumi, ni kujipotezea fursa tulizo nazo kwa
faida ya wengine. Hawa wanawasumbua nyie mwasikilize, wao shughuli zao
za NIGHT CLUBS, GUEST HOUSE ZAO, BAR ZAO, CASINO ZAO,
DALADALA ZAO, MAHOTEL, na BIASHARA ZAO
NYINGINE zinaendelea kuwaingizia Pesa na wanachofanya ni kuwajaza
matumaini ya uwongo huku wao wanajaa MAPESA. Kwa kuwa wameamua kutumika
na mataifa ya nje kuhujumu nchi yao, bado wanalipwa kwa kazi yao ya
UFITINI. Mapato yao hayayumbi na wala hayatayumba
No comments:
Post a Comment